Around the Diocese

JUBILEI YA MASISTA WA IHSA - 08/12/2018

Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma MichaeL Msonganzila amewakumbusha masista kuwa watu wa sala, ili kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu,lakini pia kumueleza matatizo yao, kwa kuwa Mungu anajibu papo kwa papo.
Askofu Msonganzila ameyasema hayo Desemba 8 mwaka huu wakati wa Misa Takatifu ya kuweka nadhili za kwanza,nadhili za daima na jubilei ya miaka 25 na 50 kwa masista wa shirika la Moyo safi wa Maria Afrika,iliyofanyika katika Kanisa la Novisiati lilopo Makoko,Jimboni Humo.
“Msiache kumbipu Mungu kupitia sala,yeye yupo kila sehemu ukimbipu tu anajipu wakati huo huo au anaweza kuchewa kidogo kukujibu ,usikate tamaa , hayo ndio maisha ya utawa,ya kuomba kila wakati na sio kusubiri mara moja kwa wiki tu” amesema Msonganzila.

Kwa upande wake Mama Mkuu wa shirika hilo Sista Maria Lucy Magumba amewashukuru Masista hao kwa kuamua kumutumikia Mungu katika maisha yao yote licha ya changamoto mbalimbali walizokumbana nazo katika maisha ya utawa,na hata wale walioweka nadhili za kwanza kwa kuamua kumtumikia Mungu ,katika maisha yao.

Pichani ni Masisita wa nadhili za daimaPichani ni Masisita wa nadhili za daima

Sista Maria Magumba aliwaomba pia wazazi na walezi kuendelea kuwaombea na kuwasaidia watoto wao ili waendelee kuimarika katika wito wao na kufanya kazi ya mwenyezi Mungu kwa upendo,na hatimaye kukamilisha kazi ya Mungu waliyoahidi kuifanya.

Na Paschal Soko Tarime.

KUTABARUKU KANISA PAROKIA YA TARIME - 24/11/2018

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Michael Msonganzila amesema kuwa hakuna sababu ya wananchi wa wilaya ya Tarime kuwa na kanda maalum ya mkoa wa Kipolisi ya Tarime/Rorya,bali wananchi hao wanapaswa kuishi maisha ya kupendana,kuheshimiana na kuwa na umoja.
Askofu Msonganzila ameyasema wakati wa Misa Takatifu ya kutabaruku Kanisa, iliyofanyika katika Parokia ya Tarime jimboni humo na kupewa hadhi ya Kanisa dogo la Kiaskofu ndani ya udekano wa Tarime, kanisa hilo la kihistoria limejengwa ndani ya mwaka mmoja kwa zaidi ya shilingi Milioni mia saba na lina uwezo wa kuchukua waamini wasiopungua elfu moja na mia tano kwa wakati mmoja.
“hatuna sababu ya kuwa na kanda maalum ya kipolisi ya Tarime/Rorya ni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yetu ya kutotaka kuheshimiana na kuonyeshana upendo neno la Mungu ni silaha tosha yakupambana na maovu ya kiroho na kimwili, pia huleta upendo, umoja na mshikamano baina ya mtu na mtu. na endapo neno la Mungu lingetumika ipasavyo kwa watu wake , kusingelikuwa na maovu duniani na watu wangeishi kwa upendo, mshikamano na amani nawaombeni sana, watumishi wa Mungu tufanye neno la Mungu kuwa nguzo pekee ya amani”Alisema Askofu Msonganzila.
Paroko wa Parokia ya Tarime Padri Lucas Chacha amesema kuwa wanaamini wanahitaji kusameheana, kutokuwekeana vikwazo vyovyote iwe kisiasa,kidini na kijamii, kupendana na kuwa na umoja ili kumtangaza Kristu.

BALOZI APONGEZA KANISA KWA KUPAMBANA NA MILA POTOFU

Balozi wa Baba Mtakatifu nchini na Askofu Mkuu Marek Solczynski amelishukuru Kanisa katoliki kwa kuendelea kutoa elimu juu ya madhara ya mila potofu ,hasa ukeketaji wa watoto wa kike, ndoa za utotoni na ndoa za mitaala.
Akizungunza na kiongozi mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kichungaji ya siku 8 ndani ya Jimbo la Musoma balozi huyo alisema kuwa, kuna baadhi ya udekano alizotembelea na amekutana na changamoto kubwa ,ya kupewa taarifa ya kuwepo kwa vitendo vya ukeketaji wa watoto wa kike,ndoa za utotoni na ndoa za mitaala ambazo zimekuwa changamoto kubwa kwa wakristo walio wengi haya kushindwa kupata sakramenti takatifu ya ndoa kutokana na wake wengi.
"Nimefika nimeona Mimi mwenyewe kwa macho yangu ,nimesikia kutoka katika taarifa zilizowasilishwa kwangu na mapadri wa udekano wa Tarime,Rorya na Serengeti ,awali nilikuwa nasoma kwenye vyombo vya habari ila nimewaona na waamini wetu hivyo,ninalishukuru kanisa kwa kuendelea kupambana na changamoto na Mungu atawasaidia na sisi tunazidi kuwaombea" alisema Balozi huyo.
Askofu wa Jimbo la Musoma Michael Msonganzila ,alisema wanamshukuru sana Balozi na Askofu mkuu kwa kuja kutembea na kuonana na waaamini wa Jimbo la Musoma ,sambamba na kujionea changamoto ambazo wanakumbana nazo katika uinjilishaji.
Mkuu wa udekano wa Serengeti ambapo ndipo alipohitimishia ziara yake ya kichungaji na kupata fursa ya kutembelea hifadhi ya wanyama ya Serengeti na kubariki hoteli na waaamini wanaoishi ndani ya hifadhi,Padri Medard Chegere alisema kuwa ujio wa Balozi huyo umewaimarisha zaidi waamini kiroho, kwani viongozi hao wanapofika katika maeneo yao ya kichungaji wanawasaidia kuinuka kiima zaidi.
Padri Chegere alisema wanachotakiwa waamini ni kuishi kwa kufuata mafundisho ya kristo,na ubatizo hivyo kufuata msingi ya imani kutokana na mafundisho ya ubatizo. Veronica Modest.

KANISA LILILOJENGWA KWA MIAKA 20 LATABARUKIWA

Waamini wa Parokia ya Shirani Jimboni Musoma wamepongezwa kwa kukua kiimani,na ushirikiana kwa pamoja katika kujitolea kufanya kazi ya Mungu ya ujenzi wa Kanisa uliodumu kwa muda wa miaka 20 bila kukata tamaa.
Pongezi hizo zimetolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma Michael wakati wa kutabaruku Kanisa hilo lililoanza ujenzi wake tangu mwaka 1998 na hatimaye kutabarukiwa hivi karibuni,huku akitangaza kuwa kituo cha hija kwa ajili ya watu wa udekano wa Rorya.
“naomba niwapongeze kwa moyo wenu wa uvumilivu wa kujitolea pasipo kuchoka,kwani tangu kanisa hili lianze ujenzi wake limechukua muda mrefu sana hadi leo hii kutabarukiwa rasmi,miaka 20 sio mchezo ni umri kabisa wa mtu mzima ,na ninyi hamkurudi nyuma mmejitahidi hadi limeisha kwa mwendo huohuo wa taratibu”amesema Askofu Msonganzila.
Amewaomba pia kutumia kanisa hilo ambacho ni kituo cha hija kufika mahali hapo mara kwa mara kwa ajili ya kusali,na kumueleza Mungu mahitaji yao,lakini pia kuomba huruma ya Mungu ,ili kuendelea kuimarika zaidi kiimani.
Paroko wa Parokia ya Shirati padri Konrad Caputa amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kwa hatua nzuri iliyofikiwa ya ujenzi wa kanisa hilo,pia anamshukuru Mhashamu Baba Askofu kwa kukubali kutabaruku kanisa hilo ambalo nila kihistoria, kutokana na kujengwa kwa muda mrefu.
Padri Caputa amesema kanisa hilo litaendelea kuw msaada mkubwa kwa kuwasaidia waamini wa Parokia hiyo ,kujijenga zaidi kiroho na kimwili,kwani awali walikuwa na kanisa dogo ambalo lilikuwa halikidhi mahitaji ya waamini hasa wanapokuwa wanahitaji kusali pamoja kwa wakati mmoja.

Veronica Modest.

PADRI JAMES CONARD AWATUMIKIA WAAMINI KWA MIAKA 40

Waamini wa Parokia ya kowak Jimboni Musoma wameombwa kusomesha watoto wao hususani wa kike ,ili waweze kujikwamua kimaisha kupitia elimu na sio kuacha watoto waolewe bila kuwa na msingi mzuri wa maisha.
Kauli hiyo imetolewa na padri James A.Conard ,wakati wa Misa Takatifu ya kumushukuru Mungu kwa kumjalia kukaa katika Parokia kwa muda wa miaka 40 tangu 1978 hadi 2018 ,lakini pia kuwaaga rasmi waamini wa Parokia hiyo kwa ajili ya kurudi nyumbani kwao nchini Marekani.
"Naomba sana msingi wa elimu niliouacha kuhusu elimu kwa watoto wa kike muuendeleze,wazazi zingatieni hilo ,hakikisheni mnakagua madaftari yao kila Mara wanapotoka shuleni,ili muendelee kupata madaktari wazuri,waalimu ,viongozi mbalimbali wanaotoka katika maeneo yenu,na sio kusubiri watu wengine waje kuwafundishia watoto wenu wakati ninyi mnawaozesha kabla ya wakati" amesema Padri Conard.
Akizungumza kwa niaba ya Mhashamu Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma,Katibu wa Askofu Padri Cleophas Sabure amesema kuwa,wanamshukuru sana kwa majitoleo yake, na kuwa na moyo wa uvumilivu ndani ya miaka 40 ,kwani amesaidia sana katika kuanzisha taasisi mbalimbali kama vile elimu,afya,miundombinu ,ujenzi wa Makanisa katika udekano wa Rorya ,vigango ,uchimbaji wa visima,pamoja na mambo mengine mengi.
Padri Sabure amesema alama aliyoiacha itakumbukwa daima kutokana na utume wake,ndani ya Jimbo hilo,lakini pia kwa kushirikiana na shirika lake la Maryknoll fathers ambalo lilimruhusu yeye kuja kufanya utume wake nchini Tanzania hususani Jimboni Musoma na watayaendeleza yale yote aliyoyaacha ,sambamba na kuendelea kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ili aendelee kumjalia afya njema huko aendako.
Paroko wa Parokia hiyo na Naibu Askofu wa Jimbo la Musoma Padri Julius Ogola amesema moyo wa utume aliouonyesha Padri Conard wa kukaa sehemu moja kwa muda wote huo unapaswa kuwa mfano wa kuigwa,kwa ni utume uliotukuka kukaa sehemu ukiwa kijana hadi ukazeeka ukiwa sehemu moja kwa muda wa miaka hiyo.
Akisoma risala kwa niaba ya waamini wa Parokia hiyo kateksta Faustine Wambori amesema kwa namna walivyoshirikiana na padri Conard katika kuwajenga kiimani,kiafya,kielimu na hata katika huduma mbalimbali za kijamii ,hawana cha kumlipa zaidi ya kumuombe kwa Mungu ili awe na maisha marefu.

Veronica Modest.

ASKOFU MSONGANZILA AWAKUMBUSHA WAKRISTO KUOMBA KILA MARA

Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma Michael Msonganzila amewakumbusha wakristo wote nchini kuwa watu wa kuomba kila mara ,kutokana na maisha ya mwanadamu kuwa , kifo ni sehemu ya kuwakumbusha waamini kuomba kabla ya kuombewa .
Askofu Msonganzila ameyasema hayo Januari 7,mwaka huu katika Kanisa la Novisiati lililopo Makoko ,wakati wa Misa ya mazishi ya Sista Maria Rita Matiku aliyefariki dunia Januai 3 mwaka huu,majira ya saa tatu na dakika ishirini(3:20) usiku ,kwa ugonjwa wa mishipa yake ya fahamu kushindwa kufanyakazi ,hali iliyoathiri uwezo wake wa kuongea na kumeza(Vocar – cords).
“Mama Rita amezaliwa 1945 na amefanya mengi sana ambayo yamebaki kuwa alama kwetu,alihimiza maendeleo ya Kiroho na Kimwili,amekuwa kiongozi kwa vipindi vitatu katika shirika,amesaidia kupatikana kwa eneo la shamba la Kitenga na sasa Immaculate Heart shule ya sekondari,Ujenzi wa makao Mkuu ya shirika-Nyarigamba Generalate ujenzi wa kanisa la Novisiati na ujenzi wa nyumba ya Emaus kwa ajili ya mikusanyiko ya Masisita”amesema Askofu Msonganzila.
Amezitaka baadhi tu ya karama alizokuwa nazo kuwa ni pamoja na kuwa na msimamo usio yumbishwa,alitenda alichokiamini kuwa sahihi na kumtegemea Mungu,kiongozi shupavu na shujaa aliweza kuwasilisha maoni yake kwa watu wa tabaka zote,alikuwa na hekima alitoa ushauri kwa aliyepokea na hata kwa yule asiyepokea,akiamini kuwa ushauri utamfaa,alikuwa mtu wa sala ,alimpenda sana YESU wa Ekaristi,alimwabudu kwa ujaji,alihimiza sala kwa msisitizo na alipenda haki na kuheshimiana.
Amesema kuwa Marehemu Sr Rita alianza kusumbuliwa na maumivu ya jicho lakini alitibiwa kwa kufanyiwa upasuaji huko Minnesota nchini Marekana na kupona,baadae 2015 iligundulika kuwa mishipa yake ya fahamu ilianza kushindwa kufanyakazi na iliathiri uwezo wa kuongea na kumeza(Vocar Cords),kuanzia 20/12/2018 hali yake ilizidi kuwa mbaya ambapo alipewa upako wa wagonjwa 21/12/2018 na mnamo 03/1/2019 saa tatu na dakika ishirini (3:20)usiku ,kwa utulivu Mungu Mwenye Huruma alimuita kwake mpendwa Mama Rita Matiku.
Akitoa salamu za rambirambi Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita Flavian Kasala ambaye ndiye aliyeeongoza misa ya mazishi ya sista huyo amesema kuwa wao wameguswa sana na msiba huyo kwani marehemu sista Maria Rita Matiku ndiye aliyeanzisha utawa wa shirika la Immaculate Heart of Sister kule Jimboni Geita,hivyo wameondokewa na mpendwa wao.
RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE SR MARIA RITA MATIKU ,APUMZIKE KWA AMANI.AMINA
Slideshow

The Road to Sainthood: Julius K. Nyerere

Sainthood. Tanzania's first president, a teacher cum politician, is held in high esteem among his countrymen. But will he become a saint?

Bishop Michael Msonganzila invites everyone across the diocese to join together in Praying for his Sainthood to be.

New Releases