Askofu MSonganzila Akemea makundi utawani


Askofu wa Jimbo katoliki la Musoma Michael Msonganzila amekemea tabia ya makundi mbalimbali yanayoanza kuibuka ndani ya watawa,ambayo amesema hayaonyeshi dalili njema kwa ustawi wa Kanisa kwani kanisa sio serikali kwamba utafukuzwa

Amesema anayejikabidhi kwa Mungu hatakiwi kuwa na ishara zozote za kutotii mamlaka , wala kuanza kusema nje kwa watu wasiohusika badala yake masuala yanapozidi ni vema yakazungumzwa na kuishia kabisa.

Askofu Msonganzila ameyasema hayo wakati wa Misa Takatifu ya kuweka nadhiri za daima , jumbilei ya miaka 25 na nadhiri za kwanza, katika Kanisa la Novisiati lililopo Parokia ya Nyamiongo Jimbo himo.

"Kanisani hatuna gereza , gereza ni dhamila yako , na nilazima uelekezwe na uelewe vizuri na usipoielewa itakudhuru mnakuelekea mnashindwa tu kusema huyu ni chama fulani cha kisiasa na huyu ni chama fulani"amesema Askofu Msonganzila.

Amesema kuna shule ambazo zimeanza kutokea za kisirisiri ambazo hazionyeshi dalili nzuri, hasa mtawa anapohamishwa kupelekwa sehemu nyingine kufanya utume, na uhamisho huwa mara nyingi sana unakuwa ni wa nia njema tu wala hauna kigugumizi cha aina yoyote,lakini maneno yatakayosikika mara baada ya kuhamishwa ndio yanayoleta mshangao mkubwa.

Amebainisha kuwa ndani ya familia pia kuna makundi ambayo hawaruhusiwi kuyatetea kama ukatili wa kijinsia au manyanyaso ya aina yoyote,hivyo yanapobainika kuwepo ni vema yakakemewa haraka sana , kabla ya kuleta adhari kimwili na kiroho.

Amewataka watawa wa kike na kiume w kuendelea kuwa na utii , wanyenyekevu,ufukara na wenye upendo ili kuendelea kufata maisha ya Kristo kama nadhili zinavyowataka kuishi.