WATAWA 11 WAWEKA NADHIRI, 2 WAFANYA JUBILEI

08/12/2021

Waamini wa Jimbo Katoliki la Musoma wamekumbushwa kuwaombea watawa wa kike na kiume ili Mwenyezi Mungu aweze kuwasaidia kutimiza nadhili zao kwa kuwa hawa ni waombezi wetu ambao wamejitoa sadaka kumtumikia Mungu.

Akizungumza wakati wa Misa Takatifu ya kuweka nadhiri za daima kwa masista watu ,nadhiri za Kwanza masisita 11 na Jubilei ya miaka 25 masisita wawili,ambayo imefanyika desemba 8 mwaka huu,katika Kanisa la Novisiati Makoko na kuongozwa na Naibu wa Askofu Padri Julius Ogolla amesema Kanisa linajivunia kupata waombezi wapya.

"Kanisa linajivunia sana kupata waombezi wengine ambao wameamua kujitoa sadaka katika maisha yao yote ,tusiache kuwaombea pia ,kwa kuwa kila mmoja anahitaji Sala za mwenzake.

Padri Ogolla amewakumbusha waamini wa Jimbo hilo umuhimu wa kuachana na dhambi,kwani dhambi inatufanya tusiwe huru kwani baada ya kutenda dhambi uhuru wote unaondolewa na hivyo kubaki uchi hali ambayo inatuweka mbali na Bwana wetu Yesu Kristo,hivyo ni vema kujiweka huru ili tusinyimwe neema kutoka kwa Mungu.

Amewaomba waamini na masista wote wakiwemo wanaoweka nadhiri kuishi maisha ya kukataa dhambi kwa kuwa bila kujiweka karibu na Mungu tunaweza kushindwa na kutufanya tusifike Mbinguni hivyo tuna kila sababu ya kutangaza imani yetu bila hofu.

Akitoa neno la shukrani mama Mkuu wa shirika la Moyo safi wa Maria Africa(IHSA) Sr. Maria Lucy Magumba amewashukuru wazazi/walezi kwa kuwatoa watoto wao ili waendelee kumtumikia Mungu na Kanisa, zaidi amewaomba waendelee kuwaombea na kuwatia moyo pale wanapokutana na changamoto katika Utume wao.

Akiwakaribisha na kuwapongeza masista wote walioweka nadhiri za Kwanza, Daima na Jubilei Mama Magumba amewataka waendelee kumtumikia vema mchumba wao waliomchangua Bwana wetu Yesu Kristo katika moyo safi na kweli ili kufikia Utume wao.

Wakitoa neno la shukrani masista wa nadhili za Kwanza, daima na Jubilei wamemshukuru Mhashamu Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma Michael Msonganzila, Mama mkuu wa shirika la Moyo safi wa Maria Africa Maria Lucy Magumba,watawa wenzao, Mapadri,walezi wao na wazazi wao kwa kuwaombea hadi kufikia siku hiyo kwa bila Sala na maombi yao peke yao wasingeweza.


Na Veronica Modest Musoma.