Walei onyesheni ukomavu miaka 50 ya Halmashauri ya walei Askofu Msonganzila

03/04/2019
Askofu wa Jimbo katoliki la Musoma Michael Msonganzila amesema kanisa haliwezi kuwa kanisa kama halina utume wa walei ambao ni wa lazima.

Askofu Msonganzila ameyasema hayo Aprili 3 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa maadhimiaho ya semina ya viongozi walei katika Jubilei ya miaka 50 ya halmashauri ya walei nchini Tanzania.

Sehemu kubwa ya uinjilishaji ni wa walei kwani walei ni kundi kubwa sana kuliko la wakilelo na tuwaite ni walei kuwa ni sehemu ya mwili wa kristo kwamba wanaalikwa daima kuonyesha uhai na utume wao katika kuinjilisha neno la Mungu.

"Ninyi walei mkishindwa kutenda kazi zanu ipanswavyo kwa ajili ya kuutunza mwili wa kristo basi uwepo wenu hauna faida ndani ya kanisa na jamii,Hivyo muendelee kuungana ili kuonyesha faida ya uwepo wenu ndani ya hekalu la Mungu " amesema

Pia amewaasa wajione kuwa wao ni kiungo katika kanisa maana jimbo bila walei ni sawa na mwili mzima kuugua kiungo kimoja ambacho kinapotesekateseka, adhali zake ni za mwili mzima hivyo ni muhimu sana katika uwepo wenu lakini pia kiidadi na kwa kutumia kikarama ambazo mwenyezi Mungu amewajaalia.

Walei msipojikazania ninyi wenyewe au kuwakazania ,kanisa linaangamia maana mtabakia kulauminiana na mapadri kwa sababu kila mmoja ameshindwa kutimiza wajibu wake katika kusimamia shughuli mbalimbali za kanisa.

Chimbuko la nafasi ya mlei kuitwa ni kiungo katika mwili wa kiristo ni sakaramenti ya ubatizo ambayo inatufanya sisi zote tuwe washiriki maalum katika kirsto kama kuhani,nabii na mfalme anaye chunga watu wake,hivyo unapobatizwa unashirikishwa katika hizo kazi.

"Unapobatiza wewe unatengenezwa kuwa raia katika kanisa katoliki ili uwe na uwezo wakupokea haki zako katika kanisa na nguvu ya kutwaa majukumu ndani ya kanisa na wajibu wako kisheria.

Aidha amesema kuwa kuna haki za jumla ambazo ni wajibu wa mlei katika kanisa ambapo walei wote wanaagizwa na Mungu kwa njia ya upatizo na kipaimara kufanyakazi kama watu binafsi au ujumla au makundi ili wokovu wa kristo ujulikane na kupokelewa na mwanadam duniani,kuutakatifuza ulimwengu,walei walioko katika sakramenti ya ndoa wanapaswa kusimama imara a kuwa mstali wa mbele katika kutimiza wajibu wao ndani ya kanisa.

Makamu Mwenyekiti wa halmashuri ya walei jimbo la Musoma Alex Kisurura amesema wanamkushuru baba Askofu kwa kuja kuwafungulia semina yao na wao viongozi wa walei wataendelea kushirikiana pamoja ili kujenga kanisa la Mungu.

Katibu wa Halmashauri ya walei Jimbo la Musoma Richard Gitenyi amesema lengo la kukutanisha viongozi wa walei kutoka jimbo zima ni kutaka kuwakumbusha umuhimu wa walei katika kanisa na wajibu wao katika kumtumikia Mungu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa idara ya kichungaji Jimbo padri Alfred Kwene amesema kama kanisa wataendelea kuwaelimisha walei namna ya kushiriki masuala mbalkmbali katika kanisa kwani ni jukumu lao katika kutumikia kanisa na chachu ya maendeleo ya kanisa na jimbo kwa ujumla.