MCHANGO WA BABA MTAKATIFU BENEDICTO WA XVI KWA NCHI ZA AFRIKA


Moja ya mchango mkubwa wa Papa Mtakatifu Benedicto wa XVI kwa Jimbo Katoliki la Musoma ni kumteua Mhashamu baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma Michael Msonganzila mnamo tarehe 10.11.2008 kuwa Askofu wa Jimbo hilo.

Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma Michael Msonganzila amesema, katika uongozi wake ndiye aliyemuona kuwa anafaa kuwa Askofu wa jimbo la Musoma na kumteua ili kuziba nafasi hiyo baada ya kifo cha aliyekuwa Askofu wa Jimbo hilo Askofu Justine Samba.

“Kwa kweli Papa Mtakatifu ana mchango mkubwa sana kwa nchi za Afrika,ameteua maaskofu wengi hasa kwa Majimbo ya hapa kwetu Tanzania,na hata nchi zingine za Afrika hivyo kuna mambo mengi mazuri na makubwa aliyoyafanya kwa nchi za Afrika. ”