WATUMISHI WAKUMBUSHWA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI-PADRI MAPAMBANO


Wafanyakazi wa Jimbo Katoliki la Musoma wamekumbushwa kuzingatia maadili sehemu ya kazi ,pamoja na kuhakikisha wanafanya kazi kwa kujituma na weledi ili kuleta ufanisi kwa Jimbo na jamii inayowazunguka.

Kauli hiyo imetolewa na Padri Augustino Mapambano wakati wa Misa Takatifu ya kila Wiki kwa wafanyakazi wa Jimbo hilo ,ikiwa ni kuelekea siku ya Mei Mosi mabayo wafanyakazi wa Jimbo hilo wanaungana na wafanyakazi wengine inchini kusherehekea siku hiyo muhimu kwao.

“ naomba niwakumbushe mambo muhimu ya kuzingatia tunapoelekea siku ya wafanyakazi,kwanza maadili ,pili weledi na tatu kujituma sana ,hii sio kwa masilahi ya mtu binafsi tu bali hata kwa Taasisi kubwa kama hii tunayoitumika ,kiroho na kijamii ,maana wengine kuna wakati wanajisahau kuwa wanapaswa kufanya nini ,wapi na kwa wakati gani ,hivyo ni vema tukaendelea kukumbashana wajibu wetu” amesema Padri Mapambano.

Ameongeza kuwa Taasisi ya Jimbo ni sehemu pia ya jamii kuiga namna bora ya ya utendaji kazi wetu sio tu kwa maneno hata matendo yetu yajidhihirishe tunapokuwa huko nje ya eneo la kazi ili kwetu utumishi wetu uweze kuaksi namna na mienendo bora ya watumishi wa Jimbo Katoliki la Musoma.

Akizungumzia kuelekea siku hiyo ya wafanyakazi ,Afisa Utumishi wa Jimbo hilo Archard Rwamunwa amesema kuwa siku ya wafanyakazi ni siku ya kujitadhimini kila mmoja wake namna anavyofanyakazi katika idara yake na namna anavyoshirikiana pia na wafanyakazi wenzake katika Ofisi hizo ,hivyo ni vema tukasherehekea kwa umoja na upendo kama sehemu ya kuwa na mahusiano mazuri .

Monica Keraryo Mratibu kitengo cha Akina mama na maendeleo,vijana na watoto Jimbo (WID GAD)amesmea siku ya wafanyakazi ni siku ya kuhakikisha pale ambapo mfanyakazi hatatimiza wajibu wake ajipange upya ili kuleta ufanisi zaidi katika ofisi na taasisi kwa ujumla.