Misa na Watumishi wa Makao makuu ya Jimbo: Zingatieni Maadili ya Kazi - Askofu Msonganzila

04/01/2024

Watumishi nchini wamekumbushwa wajibu wa kufanyakazi kwa kuzingatia maadili ya kazi, kufata sheria na kuwa waaminifu katika mazingira yao ya kazi sambamba na kutoa huduma iliyo bora ili kuendelea kuaminiwa na waajili wao lakini pia jamii inayowazunguka.

Kauli hiyo imetolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma Michael Msonganzila wakati wa adhimisho la Misa Takatifu ya alhamisi ya kwanza ya mwaka 2024 kwa watumishi wa makao makuu ya Jimbo hilo,ambapo ni kawaidia kwa watumishi wa makao makuu ya Jimbo hilo kuwa na Misa Takatifu kila alhamisi ya wiki kabla ya kuanza kazi.

Askofu Msonganzila amesema suala la kuzingatia nidhamu na weledi mahali pa kazi ni muhimu sana hasa kwa kutambua kuwa utoaji mzuri wa huduma nzuri ndio utakaosaidia watumishi kulitangaza neno la Mungu kupitia nafasi na vitengo mbalimbali wanavyovisimamia ndani ya Jimbo.

Flowers in Chania

Askofu Msonganzila amesisitiza zaidi suala la kusameheana na kudumisha amani miongoni mwao kwa kuwa msamaha ni dawa ndani ya mioyo yao,na kwamba unaposhindwa kumsamehe mwenzako unajiweka mbali na Baraka za Mwenyezi Mungu, na hivyo kushindwa kutimiza malengo yako kwa kuwa kutofanikisha baadhi ya mambo,ambapo amewaomba kuwa watu wa tafakari juu ya mambo yaliyofanyika mwaka jana, ili kubadilika na kuyaacha yale yote maovu.

tutafute kuwa wadau wa amani,tukianza na sisi wenyewe kila mmoja ajitafakari kwanza na tunapoongelea kuwa mdau wa amani tunaongelea kuwa waadilifu, wapole, wanyenyekevu, wasikivu,wapatanishi na wanaokubali kukaa na wenzao. lakini pia kusema samahani kwa hili nililolitenda, Ndugu zangu msamaha umepotea kati yetu na katika makundi mengi, ndio maana kuna fujo nyingi katika jamiiAmesema Askofu Msonganzila.

Ofisa Utumishi wa Jimbo hilo Archard Rwamunwa amemshukuru Mhashamu Baba Askofu wa Jimbo hilo kwa kukubali kuja kuadhimisha Misa Takatifu ya kwanza ya mwaka 2024 ya kumshukuru Mungu kwa kutuvusha salama na watumishi wa Jimbo hilo lakini pia kuwapatia neno la kuwatia moyo wafanyakazi wa makao makuu ya Jimbo hilo ambalo lina zaidi ya watumishi 46.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi hao,Mwenyekiti wa Watumishi wa makao makuu ya Jimbo na Mratibu wa kitengo cha Women in Development Jimbo la Musoma (WID GAG) Monica Daniel amemshukuru Mhashamu baba Askofu kwa kuanza mwaka mpya pamoja na watumishi hao na ahadi yao kwa mwajili wao ambaye ni baba Askofu ni kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi ndani ya Kanisa Katoliki,ili kuendelea kumtangaza Kristo katika utendaji wao na namna wanavyotoa huduma kwa jamii inayowazunguka.